Machapisho

MANENO MAZITO YA NAY WA MITEGO KUHUSU MAISHA YAKE

Picha
Siku kadhaa zimepita tangu msanii Nay wa Mitego kuachiwa huru, ambapo alikuwa akishikiliwa na Jeshi la polisi kwa tuhuma za wimbo wake wa  ‘WAPO’  kudaiwa kutokuwa na maadili. Msanii Nay wa Mitego aliachiwa huru baada ya agizo la Rais Dk. John Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Dk. Harrison Mwakyembe lakine leo April 3 2017 Nay kupitia instagram account yake ameandika maneno yanayoashiria kuwa hayuko katika hali ya usalama. “Usalama wa Maisha yangu umekuwa Mdogo kwa sasa, Wanapanga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii Dunia. Nipo tayari kwa chochote wanachopanga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni Mwana Muziki si vingine” “Kwa chochote kitachotokea Familia yangu itakuwa na chakuongea, Siwezi kuhama Nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa na siko tayari kupindisha Chochote.! Nyie Ndo ...

SEIF AMTOLEA NJE LIPUMBA CUF

Picha
                                             SEIF AMTOLEA NJE LIPUMBA CUF Sarakasi za kisiasa zinaendelea kutawala ndani ya chama cha CUF baada ya Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad, kudai kuwa Profesa Ibrahim Lipumba anatumiwa kukihujumu chama hicho. Maalim Seif alimtuhumu Profesa Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa CUF, anayetambuliwa na ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuwa anakihujumu chama ili kishindwe kudai haki waliyoipata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka juzi. Aliyasema hayo jana katika kijiji cha Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja alipozungumza na wanachama wa chama hicho, ikiwa ni ziara maalumu ya uimarishaji wa chama katika mikoa yote ya Kisiwa cha Unguja. Maalim Seif alisema pamoja na Profesa Lipumba kupata ng...

MWENGE WA UHURU WAANZA KAZI RASMI

Picha
Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2017 zimezinduliwa rasmi jana katika uwanja wa Kumbukumbu Mjini Mpanda mkoani Katavi na unatarajiwa kuzunguka katika mikoa yote 31, ukipita kwenye halmashauri 195 kwa muda wa siku 195. Katika sherehe hizo za uzinduzi, kiongozi wa mbio hizo kwa mwaka huu pia ametangazwa rasmi, ambapo atakuwa ni Amour Amad Amour kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar. Kiongozi huyo atasaidiana na wenzake watano katika kukimbiza mwenge huo ambao ni pamoja na Bahati Mwaniguta Lugodisha (Geita), Bi Fatima Yunus Hassan (Kusini Pemba), Fredrick Joseph (Singida), Salome Obadia Mwakitalima (Katavi) na Shukran Islam Msumi (Mjini Magharibi). Kauli mbiu ya mbio hizo kwa mwaka huu inasema "SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU' Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi Seif Ali Idd kwa niaba ya Rais wa serikali hiyo Dkt. Ali Mohamed Shein, ambapo...

ALIYETUMBULIWA NA MAGUFULI AULA UN

Picha
Salamu za pongezi zimeendelea kumiminika kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (Nimr), Dk Mwele Malecela baada ya kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika vya Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika. Pia, Dk Mwele  aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Mpango wa Maalumu wa WHO wa kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele (Espen) na sasa atahamia kituo chake cha kazi Congo-Brazaville.  Mradi wa Espen ulianza kutekelezwa mwaka 2016 hadi 2020, una lengo la kumaliza magonjwa yasiyopewa kipaumbele kwa kutoa vifaa tiba, elimu na dawa.  Magonjwa yasiyopewa kipaumbele ni pamoja na matende, mabusha, kichocho, minyoo ya tumbo na usubi.  Miongoni mwa waliomtumia pongezi ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Sikika, Irenei Kiria ambaye aliandika katika ukurasa wake wa Twitter: “Hongera Mwele kwa kupata nafasi hiyo ina maana ulipangwa kulisaidia Taifa letu ukiwa nje.”  Mwingine...

ZITTO AGONGA MWAMBA UBUNGE EALA

Picha
      ZITTO AGONGA MWAMBA UBUNGE EALA     Mbunge  wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo),  amegonga mwamba baada ya Kamati ya Kanuni ya Bunge kutoa msimamo wake kuhusu uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Hatua hiyo inatokana na Zitto kuwasilisha barua kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, Machi 28, mwaka huu akitaka kamati hiyo kutoa ufafanuzi wa mgombe wa kundi C ili kila chama kiweze kushiriki uchaguzi, badala ya kupewa kwa vyama vilivyokuwa na idadi kubwa ya wabunge. Kutokana na Tangazo la Bunge kwenye gazeti namba 11 la Machi 17, lililotangaza uchaguzi huo na masharti yake, Zitto, alisema mwongozo wa uchaguzi huo unavunja kanuni mbalimbali na kwamba kitakachofanyika sasa kitakuwa ni uteuzi na si uchaguzi. Alisema pia mwongozo huo, mbali na kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, unaotaka suala la jinsi lizingatiwe kwenye wabunge wanaokwenda kuiwakilisha nchi katika Bunge hilo, ...